Polisi waimarisha oparesheni ya kuwarejesha mifugo walioibiwa eneo la Moite.
NA HENRY KHOYAN
Polisi wamethibitisha kuwa wameimarisha oparesheni ya kusaka mifugo iliyoporwa katika eneo la Moite wiki iliyopita.
Takriban wiki moja baada ya wizi huo, maafisa wa usalama kwa kushirikiano na jamii za eneo hilo wanaendelea na msako dhidi ya wahalifu na mifugo hiyo.
Naibu Kamishna wa kaunti ndogo ya North Horr, Tobias Onyango Okoth, amesema jamii husika imeomba hadi Jumapili ili kusaidia kufanikisha upatikanaji wa mifugo hiyo.
Aidha, Okoth amesema wezi hao huenda wamejigawa sehemu mbili, na polisi bado wanaendelea kuwafuatilia kwa karibu ili kuhakikisha mifugo inarejeshwa kwa usalama.



Post Comment