Mshukiwa wa uavyaji mimba afikishwa mahakamani Marsabit
Mwanaume mmoja anayeshukiwa kutekeleza uavyaji mimba katika eneo la Dirib Gombo kaunti ya Marsabit amefikishwa mahakamani mbele ya hakimu mkuu mwandamizi Christene Wekesa.
Mahakama hiyo imeelezwa kuwa mshukiwa Harun Muthuri alitekeleza kosa hilo katika kituo chake binafsi cha matibabu mwanzoni mwa mwaka huu ila amekana mashtaka dhidi yake.
Wakati uo huo Muthuri anakabiliwa na hatia nyingine ya kuvamia maafisa wa polisi na kumjeruhi mmoja wao.
Hakimu Wekesa ameamuru kufanyiwa ukaguzi wa kiakili na ripoti kuwasilishwa mahakamani tarehe 12 mwezi huu wakati kesi hiyo itakapotajwa tena.
Kwa sasa mshukiwa anazuiliwa rumande katika kituo cha polisi cha Marsabit.



Post Comment