Maafisa 87 wa usalama kaunti ya Marsabit wapokea mafunzo kuhusu afya ya akili.
NA JB Nateleng
Zaidi ya maafisa 87 wa usalama Marsabit wamepokea mafunzo kuhusu afya ya akili kwa lengo la kupunguza visa vya kujitoa uhai vinavyo aminika kuletwa na msongo wa mawazo.
Akizungumza na wanahabari hii leo, mkuu wa idara ya uchaplaini katika idara ya polisi Francis Kooli amesema kwamba idara hii imebuni mikakati ya kutoa hamasa kwa polisi kuhusu msongo wa mawazo, ili kuwasaidia maafisa wa usalama kupata muongozo ambao utawasaidia wanapokumbana na changamoto kazini.
Kooli amesema kuwa mpango huu ulianzishwa baada ya ongezeko la visa vya kujitoa miongoni mwa maafisa hao
Francis pia amewapachangamoto maafisa wa usalama kuzungumza na wenzao wanapokumbana na msongo wa mawazo ili waweze kupata msaada wa dharura.
Kwa upande wake mchungaji kutoka kanisa la CITAM Rev Evans Agoya ameitaka jamii, mashirika ya kidini pamoja na mashirika yasiyokuwa ya kiserekali kuja pamoja na kuwasaidia maafisa wa usalama wanaokumbwa na msongo wa mawazo,
Itakumbukwa kwamba mapema wikii hii Afisa mmoja wa polisi alijiua kwa kujipiga risasi katika eneo la Forolle eneobunge la NorthHorr kaunti ya Marsabit kutokana na kile kinachoaminika kuwa ugomvi pale nyumbani.



Post Comment