Loading Now

Highlights

Kongamano la vijana Marsabit lasisitiza amani na uwajibikaji

Na JB Nateleng

Kongamano la vijana wa kaunti ya Marsabit limefanyika leo Jumatano katika eneo bunge la Saku.

Kongamano hilo ambalo limeandaliwa na shirika la Initiatives for Progressive Change (IFPC), limewaleta pamoja viongozi wa vijana katoka ya Saku, Moyale, North Horr na Laisamis, pamoja na idara za kaunti, asasi za kiraia na wadau wengine.  

Akizungumza na wanahabari mkurugenzi wa shirika la IFPC Hassan Mulata amesema kwamba kongamano hili litasaidia katika kushinikiza serekali ya kaunti kubuni sheria zitakazo kutetea haki ya vijana.

Mulata pia anasema itakuwa afueni iwapo vijana watapewa nafasi ya kupatana na viongozi wao kama njia moja ya kuendeleza uwazi na uwajibikaji katika masuala ya uongozi na matumizi ya rasilimali ya umma.

Wakati uo huo Mulata ametaja upana wa kaunti ya Marsabit kuwa changamoto kuu ya kuwafikia vijana wote.

Lavin Atieno kutoka kwa shirika la Prospect Peace Institute Africa, amesema kwamba kongamano kama hili linasaidia kuhakikisha kwamba vijana wanahamisishwa kuhusu umuhumi wa amani, umoja pamoja na kujua mbinu ya kuwashinikiza viongozi kuwajibikia majukumu yao.

Post Comment