Loading Now

Highlights

Kesi za unajisi pamoja na ulawiti zazidi kuongezeka Marsabit

NA Caroline Waforo

Kesi za unajisi zimeongezeka katika mahakama ya Marsabit huku washukiwa wakuu wakiwa ni watu wa karibu na waathiriwa.

Aidha, mahakama hiyo pia imerekodi ongezeko la kesi za ulawiti, hali inayozua wasiwasi mkubwa miongoni mwa wadau wa haki na ustawi wa jamii.

Akizungumza na wanahabari afisini mwake, Hakimu Mkaazi wa mahakama ya Marsabit Christine Wekesa, amesema ongezeko la visa hivyo linachangiwa na mila na tamaduni zilizopitwa na wakati, utepetevu wa wazazi katika malezi pamoja na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Hakimu Wekesa amesisitiza umuhimu wa kuhamasisha jamii kuhusu maswala ya sheria, akisema kuwa ulewa mdogo umesababisha visa vya uharibifu wa ushahidi hali inayoweza kuathiri upatikanaji wa haki kwa waathiriwa.

Kutokana na ongezeko la visa vya unajisi na hata ulawiti Hakimu Wekesa amesema kuwa ipo haja ya serikali ya kaunti kwa ushirikiano na serikali kuu na wadau wengine kuchukua hatua za haraka kujenga makazi salama ya kuwahifadhi waathiriwa wa visa hivyo.

Haya yanajiri huku nyingi ya kesi hizi zikikosa kuripotiwa kwa hofu ya unyanyapaa.

Post Comment