Loading Now

Highlights

Gavana Mohamud Ali ahidi kutoa mazingira bora kwa  biashara za vijana Marsabit.

NA JB Nateleng

Gavana wa kaunti ya Marsabit, Mohamud Ali, amewahakikishia vijana waliopata mtaji wa kuanzisha biashara kupitia mradi wa NYOTA kuwa serikali ya kaunti itabuni mazingira bora ya kuendesha biashara zao kwa usahihi na usawa.

Akizungumza katika hafla ya utoaji wa fedha iliyoongozwa na Rais William Ruto katika Kituo cha Archers Post, Kaunti ya Samburu, Gavana Mohamud amesema kaunti ipo imara kuhakikisha vijana hao wanapata mafunzo ya kutosha na muda wa kutosha wa kuendesha biashara zao kwa njia salama na yenye tija.

Aidha, amefutilia mbali ada ya leseni ya mwaka mmoja kwa vijana hawa na kuahidi ushirikiano zaidi wa kaunti ili kuwasaidia kiuchumi.

Post Comment