Gavana Mohamud aahidi kushirikiana na vijana na kuongeza ajira Marsabit
Na JB Nateleng
Gavana wa Marsabit, Mohamud Ali, amekosoa wale wanaodai kuwa serikali yake haishughulikii masuala ya vijana.
Akizungumza alipofungua rasmi kongamano la vijana leo, Mohamud amesema serikali ya kaunti imetoa nafasi za ajira kwa vijana na kuhakikisha wanapata mazingira salama na mazuri ya kufanya kazi.
Gavana amesema hakuna kaunti nyingine nchini iliyo fanikiwa kama Marsabit katika kutoa nafasi za ajira kwa vijana.
Ameahidi kushirikiana na vijana katika masuala yanayowahusu na kuwajumuisha katika uongozi, akisema kwamba vijana ndio nguzo muhimu ya jamii imara.



Post Comment