Loading Now

Highlights

Bunge la Kaunti ya Marsabit hutenga milioni 55 kila mwaka wa kifedha kufadhili mpango wa chakula ECDE-Asema mwakilishi wadi mteule Kiya Jillo

NA JB Nateleng

Naibu Mwenyekiti wa kamati ya Elimu katika bunge la kaunti ya Marsabit Kiya Jillo ambaye pia ni mwakilishi wadi mteule, amesema kwamba bunge la kaunti hutenga shilingi millioni 55 kila mwaka wa kifedha ili kufadhili mpango wa chakula katika shule za chekechea.

Akizungumza na wanahabari hapo jana Jumatano wakati ya hafla ya kuwaajiri walimu 84 wa chekechea jimboni, Jillo ameeleza kwamba hapo awali kumekuwepo na changamoto ya usambazaji wa chakula katika shule zote za chekechea kutokana na kuchelewa kwa mgao wa fedha kutoka kwa serikali kuu.

Aidha ameipongeza idara ya Elimu ya Chekechea Marsabit kwa kufanikisha mpango huo wa chakula shuleni haswa msimu huu wa kiangazi.

Jillo vilevile ameeleza ukosefu wa madarasa ya kutosha akipendekeza kujengwa kwa madarasa zaidi ya PP1 na PP2 katika vituo vya ECDE ili kuinua hadhi ya masomo.

Post Comment