Loading Now

Highlights

Wito watolewa kwa wazazi Marsabit kuwa karibu na wanao kipindi cha likizo fupi

Na JB Nateleng

Huku wanafunzi wakitarajiwa kurejea nyumbani kwa ajili ya likizo fupi ya muhula wa kwanza wiki hii, wito umetolewa kwa wazazi kaunti ya Marsabit kuwa karibu na wanao ili kuwakuza kimaadili.

Akizungumza na Shajara, Mkurugenzi wa Elimu kaunti ya Marsabit William Kamugunah, amepongeza ushirikiano uliopo baina ya wazazi na wadau wa elimu ambao umefanikisha kuendelea kwa masomo tangu kuanza kwa muhula huu wa kwanza.

Kamugunah amesema licha ya changamoto za kiangazi kinachoshuhudiwa, idara ya elimu kwa ushirikiano na wadau mbalimbali waliweza kuhakikisha kwamba wanafunzi wanasalia shuleni na kuendelea na masomo.

Vile ile amewapa changamoto wanafunzi kuwa watiifu kwa wazazi wao na kutumia nyema muda wa likizo kwa kushiriki shughuli zitakazowajenga kitaaluma na kimaadili.

Likizo fupi itaanza siku ay Jumatano ya tarehe 25Februari na kukamilika tarehe 2 Machi 2026.

Post Comment