Wazazi wa shule ya msingi ya Comboni Marsabit waandamana kutokana uongozi wa shule hiyo kubadilishwa.
NA JOHN BOSCO NATELENG
Shughuli ya ufunguzi wa shule kwa muhula wa kwanza mwaka huu 2026 umetatizika katika shule ya msingi ya Comboni iliyoko eneo la Mlima mitatu, eneo bunge la Saku kaunti ya Marsabit baada ya wazazi wa eneo hilo kukatalia lango kuu la shule wakitaka tume ya kuajiri walimu (TSC) kutoa maelezo zaidi kuhusu uteuzi wa mwalimu mkuu mpya.
Kulingana na wazazi hawa wanahisi kwamba tume hiyo imewatenga wakati walipokuwa wanafanya uteuzi huu wakidai kwamba imeharakishwa na pia hawajahusishwa ipasavyo.
Wamesisitiza kwamba tume ya TSC inafaa kuangazia na kusikia mlalamishi pamoja na maslahi ya jamii ya eneo hilo na kuleta mtu ambaye atasaidia katika kuleta utulivu na uhusiano mwema baina ya jamii.



Post Comment