Loading Now

Highlights

Waumini wakatoliki wahimizwa kutumia wiki takatifu kwa sala na tafakari.

NA JB Nateleng

Wakati Kanisa Katoliki linaendelea kuadhimisha Wiki Takatifu, ambayo ni kilele cha kipindi cha Kwaresma, Wakristu wamehimizwa kuitumia fursa hii kuwaombea watu wote katika jamii.

Akizungumza na idhaa hii, msimamizi wa liturjia katika Jimbo Katoliki la Marsabit, Padri Emmanuel Galgidhielle, amesema kuwa Wiki Takatifu iliyoanza na Jumapili ya Matawi ni kipindi muhimu kinachopaswa kuzingatiwa kwa uzito, kwani kinaakisi mateso, kifo na ufufuko wa Yesu Kristo ambayo ni msingi wa imani ya Kanisa Katoliki.

Padri Emmanuel amewahimiza waumini kutumia muda huu kwa tafakari ya kina kuhusu mateso ya Kristo, pamoja na kujitathmini ili kubadili mienendo yao na kuwa bora zaidi.

Aidha, ameeleza kuwa Kanisa huadhimisha fumbo kuu la imani kuanzia Alhamisi Kuu hadi Jumamosi Kuu kupitia ibada na sala maalum.

Vilevile, amesisitiza umuhimu wa Ijumaa Kuu kuwa siku ya sala na tafakari, akiwataka Wakristu kukumbuka mateso ya Yesu Kristo na kuwaombea wale wanaopitia changamoto mbalimbali katika jamii.

Post Comment