Wahamiaji 6 raia wa Ethiopia washtakiwa katika mahakama ya Marsabit kwa kuwa nchini kinyume cha Sheria
Wahamiaji 6 raia wa Ethiopia wameshtakiwa katika mahakama ya Marsabit kwa kuwa nchini Kenya kinyume na sheria.
Wanaume hao 6 walikamatwa tarehe 1 mwezi huu wa Februari katika eneo la Orondel eneobunge la North Horr kaunti ya Marsabit na kuwasilIshwa mahakamani Jumatatu ya tarehe 2.
Mbele ya Hakimu Mwandamizi wa mahakama hiyo ya Marsabit Meshack Otieno, 6 hao walikiri mashtaka dhidi yao na kuomba kurejeshwa makwao.
Mahakama imewapiga faini ya shilingi 50,000 au kutumikia kufungo cha miezi 5 gerezani.
Aidha hakimu Otieno ameagiza idara ya uhamiaji kuwarejesha wanaume hao nchini Ethiopia baada ya kulipa faini au kutumikia kifungo.



Post Comment