Loading Now

Highlights

Wafugaji Marsabit walalamikia bei ya chini ya mifugo huku shule zikifunguliwa wiki ya kwanza.

NA Samuel Kosgei

Wafugaji jimboni Marsabit wametakiwa kuanza kupunguza mifugo yao kwa kuuza ili wasije wakapata hasara kiangazi kinapozidi.

Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Caritas Marsabit Isacko Jirma ameambia shajara kuwa wafugaji wanafaa kutumia fursa ambapo wanyama wana afya kuwauza kabla yao kuanza kupoteza kilo au kushambuliwa na magonjwa.

Wakati huo amewashauri kuzidi kufuatilia bei kwenye soko la mifugo. Zaidi ya hayo amewataka wafugaji hao sawa na wakulima kufuatilia ushauri wa idara ya utabiri wa hali ya hewa.

Hata hivyo, Mzee Lekupes       ambaye ni mfugaji kutoka eneo la Karare ameonesha masikitiko yake kutokana na bei ya chini ya mifugo katika eneobunge la Saku. Lekupes amerai wanunuzi wa mifugo kaunti ya marsabit kutengeneza bei ya mifugo anayosema inapungua sana wakati wa shule zinapofunguliwa.

Post Comment