Viongozi wa Marsabit waomba msaada wa chakula msimu wa kiangazi ukirindima.
NA NYABANDE ORWA
Viongozi wa kaunti ya Marsabit wametoa wito kwa wahisani na wadau mbalimbali kutoa msaada wa chakula na maji kwa wakazi wa kaunti hii, wakisema hali ya ukame imezidi kuwa mbaya.
Wakizungumza eneo la Sololo, viongozi hao wameeleza wasiwasi kwamba bila hatua za dharura, maisha ya wananchi na mifugo yako hatarini.
Naomi Jillo Waqo ni mwakilishi wa akina mama katika Kaunti ya Marsabit.
Ameongeza kuwa serikali kuu inapaswa kuimarisha mpango wa lishe shuleni ili wanafunzi waendelee na masomo bila changamoto pindi shule zitakapofunguliwa mwaka ujao.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi amesema serikali itaweka mikakati thabiti kukabiliana na njaa.
Hata hivyo, Mudavadi ameitaka jamii kumuunga mkono Rais William Ruto katika juhudi zake za kutafuta muhula wa pili kwenye uchaguzi mkuu wa 2027.



Post Comment