Highlights

Viongozi wa dini ya Kiislamu wahimiza serikali  kutoa misaada ya vyakula msimu huu wa mfungo wa Ramadhan

NA JB Nateleng

Huku waumini wa dini ya Kiislamu wakianza mfungo wa mwezi wa Ramadhan leo Jumatano, wito umetolewa kwa serikali kuu, ile ya kaunti ya Marsabit pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali kutoa misaada ya vyakula kuwafaa waumini hao ili kuwarahisishia wanapoendelea na mfungo huo.

Akizungumza na Shajara, Sheikh wa Msikiti wa Jamia hapa Marsabit Mohamed Noor amesema kuwa athari za kiangazi zinazoshuhudiwa kwa sasa zinaweza kuathiri pakubwa mfungo wa Ramadhan.

Na katika msimu huu unaotukumbusha kuhusu ubinadamu, amani, huruma na maelewano Sheikh Noor amewataka waumini wote kutowabagua wenzao wasio na chochote cha kutoa kama ishara ya shukrani.

Na kutokana na visa vya ulawiti ambavyo bado vinashuhudiwa hapa Marsabit Sheik Noor amelaani visa hivyo huku akiitaka idara ya usalama kuwakamata washukiwa na kuwawajibisha  kwa mujibu wa sheria

Post Comment