Ukavu kuendelea kushuhudiwa jimboni Marsabit- Idara ya hali ya anga yadokeza
Na JB Nateleng
Utabiri wa hali ya hewa katika kipindi cha siku saba zijazo kuanzia leo tarehe 17 Februari hadi 23 Februari 2026 unaonyesha kuwa Kaunti ya Marsabit itaendelea kushuhudia vipindi vya jua mchana, huku hali ya mawingu mepesi yakitarajiwa nyakati za usiku katika maeneo yote ya kaunti ya Marsabit.
Ripoti hiyo inaeleza kuwa joto la mchana jimboni, linatarajiwa kufikia nyuzi joto 30 huku baadhi ya maeneo katika eneobunge la Saku na Mt Kulal likitarajiwa kushuhudia kijibaridi cha asubuhi.
Aidha eneo la Loiyangalani linatarajiwa kushuhudia upepo mkali huku maeneo mengine jimboni yakipata upepo wa wastani hadi wenye nguzu kutoka Kusini hadi Kusini mashariki.
Kwa mujibu wa utabiri huo, mvua haitarajiwi kunyesha katika kaunti nzima ya Marsabit.
Wakaazi Marsabit wanashauriwa kunywa maji na kuchukua tahadhari dhidi ya jua.



Post Comment