Loading Now

Highlights

Polisi wazima maandamano ya wakazi wa Nyayo Road wanaolalamikia ubovu wa barabara

Na Nyabande Orwa

Polisi wamelazimika kuingilia kati kuzima maandamano ya wakazi wa Nyayo Road katika wadi ya Marsabit Central, waliokuwa wakilalamikia ubovu wa barabara ya eneo hilo.

Wakazi hao walikusanyika barabarani wakidai kuwa wamekuwa wakilalamikia hali mbaya ya barabara hiyo kwa muda mrefu bila hatua kuchukuliwa. Wamesema uongozi wa kaunti umekuwa ukitoa ahadi za ukarabati ambazo hazijatekelezwa.

Kwa mujibu wa wakazi, uwekaji wa MARAM si suluhisho la kudumu kwa kuwa mvua inaponyesha husombwa na maji na kuacha mashimo na mitaro. Wahudumu wa bodaboda, ambao hutegemea barabara hiyo kila siku, wamesema hali hiyo huhatarisha maisha yao na ya abiria hasa wakati wa mvua kutokana na utelezi.

Wameitaka serikali ya kaunti pamoja na mwakilishi wa wadi, Jack Elisha, kuhakikisha barabara hiyo inawekewa lami kama suluhu ya kudumu.

Hata hivyo, baadhi ya wakazi wamekosoa hatua ya kuchoma magurudumu na kuchimba barabara wakisema inazidisha uharibifu badala ya kuleta suluhu ya kudumu.

Post Comment