Loading Now

Highlights

Naibu Kamisha wa Moyale apiga marufuku ajira kwa watoto mjini humo

Na Caroline Waforo

Naibu kamishna wa Moyale kaunti ya Marsabit Benedict Munywoki, amepiga marufuku ajira kwa watoto mjini humo kutokana na hofu ya ongezeko la visa vya watoto wanaojihusisha na biashara ya rejareja.

Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara kati ya jamii na maafisa wa polisi kuhusu usafirishaji wa binadamu, DCC Munywoki amesema kuwa amri hiyo itaanza kutekelezwa rasmi siku ya hapo kesho Alhamisi.

Mapema leo wakati wa kikao hicho wakaazi mjini Moyale waliibua wasiwasi kuhusu ongezeko la visa vya ajira kwa watoto ikiwemo wanaotoka katika taifa jirani la Ethiopia.

Wakaazi hao wameitaka idara ya usalama kwa ushirikiano na idara ya watoto kuhakikisha kuwa watoto hao wanarejeshwa makawao.

Post Comment