Mwanaume mmoja afariki dunia kufuatia ajali ya barabarani, Kargi
NA CAROL WAFORO
Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 63 amefariki dunia kufuatia ajali ya barabarani ambayo imefanyika leo Jumatatu katika barabara ya Kargi kuja Marsabit.
Akithibitisha mkasa huo kamanda wa polisi katika kaunti ya Marsabit Leonard Kimaiyo amesema kuwa gari aina ya Land Cruiser lililokuwa limebeba abiria, lilishindwa kupanda mlima na kuanguka.
Aidha wasichana watatu wenye umri wa miaka 16, 17 na 19 wameachwa na majeraha kufuatia ajali hiyo.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika makafani ya hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Marsabit.
Kamanda Kimaiyo amewataka madereva kuwa waangalifu barabarani na kuheshimu sheria za trafiki haswa msimu huu ambapo wanafunzi wanarejea shuleni kwa muhula wa kwanza wa mwaka 2026.



Post Comment