Loading Now

Highlights

Mwanaume mahakamani kwa kutishia kumuua mkewe na wanawe huku mwingine akishtakiwa kwa kutishia kumuua nduguye, Marsabit.

Wanaume wawili wameshtakiwa katika mahakama ya Marsabit kwa tuhuma za kutishia kuua katika visa viwili tofauti.

Katika kesi ya kwanza, mahakama imearifiwa kuwa mnamo tarehe 8 mwezi Januari katika lokesheni ya Nagayo, kaunti ndogo ya Marsabit Central mshukiwa Wario Molu, alitishia kumuua mke wake pamoja na wanawe.

Mshukiwa alikamatwa tarehe 9 mwezi huu wa Januari na kufikishwa mahakamani leo Jumatatu mbele ya hakimu Hakimu Mkuu Mwandamizi Christine Wekesa.

Molu amekana shtaka dhidi yake kuachiliwa kwa bondi ya shilingi 100,000 au dhamana ya pesa taslimu shilingi 50,000.

Katika kesi ya pili, mshukiwa Adan Halake Babo, anatuhumiwa kutishia kumuua nduguye huku akiwa amejihami kwa kisu.

Mahakama imearifiwa tukio hilo lilitendekeza mnamo tarehe 9 mwezi Januari katika lokesheni iyo hiyo ya Nagayo.

Adan pia anakabiliwa na mashtaka mengine mawili, likiwemo shtaka la kujihusisha na tabia za kuchukiza kwa kutamka maneneo machafu kwa nia ya kuvuruga amani, pamoja na shtaka la kusababisha taharuki kwa kurusha mawe na kumfukuza mamake mzazi kwa mawe.

Leo Jumatatu, mshukiwa amekana mashtaka yote matatu mbele ya Hakimu Wekesa na kuachiliwa kwa bondi ya shilingi 100,000 au dhamana ya pesa taslimu shilingi 50,000.

Kesi zote mbili zitatajwa tena tarehe 27 mwezi huu wa Januari.

Wakati uo huo

Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 57 ameshtakiwa katika mahakama ya Marsabit baada ya kunaswa na changaa kinyume na sheria.

Mahakama imearifiwa kuwa mnamo tarehe 11 mwezi Januari katika lokesheni ya Nagayo, kaunti ndogo ya Marsabit Central, mshukiwa Adan Abdi alinaswa akiwa na lita 52 za changaa.

Mshukiwa alikamatwa jana Jumapili na kuwasilishwa mahakamani leo Jumatatu mbele ya Hakimu Mwandamizi Christine Wekesa.

Mshukiwa amekana mashtaka dhidi yake na kuachiliwa kwa bondi ya shilingi 50,000 au dhamana ya pesa taslimu 30,000.

Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 27 mwezi huu wa Januari.

Post Comment