Loading Now

Highlights

Mvua yaongeza kiwango cha maji bwawa la bakuli

Na Nyabande Orwa.

Maji katika bwawa la bakuli, kaunti ya Marsabit, sasa yamefikia nusu. Hayo ni kulingana na Mkurugenzi wa Kiufundi wa kampuni ya usambazaji maji kaunti hiyo, MARWASCO, John Alkano.

Akizungumza na kituo hiki, Alkano amesema mvua zilizonyesha hapo awali hazikuchangia kujaa kwa bwawa hilo kutokana na uchache wake. Hata hivyo, mvua iliyonyesha wiki jana iliingia kwenye bwawa na kusaidia kuongeza kiwango cha maji.

Amesema hali kwa sasa si mbaya ikilinganishwa na ilivyokuwa hapo awali.

Wakati huo huo, Alkano amesema kiwango cha maji kinachosambazwa kimepungua, kutokana na msimu wa mvua ambapo wananchi wengi wanatega maji majumbani mwao.

Aidha, amesema MARWASCO inaendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha kunakuwa na vyanzo mbadala vya maji wakati wa kiangazi, ikiwemo kuwekeza kwenye visima vya maji.

Post Comment