Mtu aaga dunia, wengine 7 wakipata majeraha baada ya gurudumu la gari kupasuka eneo la Gof Choba Marsabit.
Mtu mmoja amefariki dunia na wengine saba kupata majeraha kufuatia ajali ya barabara iliyotokea asubuhi ya leo katika eneo la Gof Choba, barabara kuu ya Marsabit – Moyale eneobunge la Saku.
Akidhibitisha ajali hiyo, OCPD wa Marsabit Central Beethoven Gachago amesema kuwa gari hilo lilipoteza mwelekeo na kubingiria baada ya gurudumu lake la mbele kupasuka.
Gari hilo lililokuwa likibeba watu wanane wa familia moja lilikuwa likienda eneo la Walda kutoka hapa Marsabit kabla ya tukio hilo kufanyika saa nne asubuhi.
Wakati uo huo OCPD Gachago ametoa taadhari kwa madereva wa magari ya umma kuendesha magari kwa uangalifu huku akiwataka kungalia magari yao vyema kabla ya safari, kutotumia vileo na hata kutobeba abiria kupindukia



Post Comment