Highlights

Gavana wa Marsabit Mohamud Ali afanya mabadiliko katika baraza la mawaziri.

Na Samuel Kosgei

Gavana wa kaunti ya Marsabit Mohamud Ali amefanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri.

Aliyekuwa waziri wa maji Grace Galmo amehamishiwa wizara ya ardhi, nyumba na ukuaji wa mji, Adan Hirbo amehamishiwa wizara ya uchukuzi na barabara kutoka ile ya ardhi huku Guyo Guracha akichukua wizara ya maji, mazingira na mali asili.

Kulingana na kaimu katibu wa kaunti na mkuu wa wafanyakazi Dr. Arero Halkano mabadiliko hayo yanaanza kutelekezwa mara moja.

Mapema leo Gavana Mohamud Ali aliongoza kikao cha 89 cha Kamati ya Utendaji ya Kaunti ya Marsabit kujadili kwa kina kuhusu hali ya ukame jimboni.

Kamati hiyo ilichambua kuhusu usambazaji wa chakula cha msaada pamoja na mipango ya dharura katika sekta mbalimbali zikiwemo maji, afya, kilimo na mifugo, pamoja na elimu.

Katika sekta ya elimu, kamati hiyo ipia ilizungumzia hali ya vituo vya elimu ya awali (ECDE) na vyuo vya ufundi vya kaunti.

Vilevile kikao hicho kilijadili makadirio ya bajeti ya ziada ya Kwanza kwa mwaka wa fedha 2025/2026 pamoja na mapitio na mwelekeo wa Bajeti ya Kaunti 2025, hatua inayolenga kuimarisha nidhamu ya matumizi ya fedha za umma.

Post Comment