Loading Now

Highlights

Watoto wanaougua kisukari Marsabit waelimishwa kuhusu udhibiti wa ugonjwa huo

Na Caroline Waforo

Kituo cha kudhibiti ugonjwa wa kisukari nchini kwa ushirikino na Idara ya Afya katika kaunti ya Marsabit, kimewaleta pamoja watoto wanaougua ugonjwa wa kisukari kutoka maeneo mbalimbali ya kaunti, ili kuwaelimisha kuhusu namna bora ya kudhibiti ugonjwa huo na kuziba pengo la maarifa linaloweza kusababisha madhara makubwa.

Hafla hiyo imefanyika katika shule ya upili ya Moi Girls, ambapo afisa kutoka kituo hicho Anthony Omondi amesema kuwa takriban wagonjwa 100 wa kisukari aina ya Type 1 wamehusishwa pamoja na walezi wao.

Kulingana na Omondi wagonjwa wa kisukari katika kaunti ya Marsabit bado wanakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo hali ngumu ya maisha pamoja na ukubwa wa jimbo hili, hali inayofanya upatikanaji wa huduma kuwa ngumu.

Aidha Omondi amehimiza wananchi kusitisha unyanyapaa dhidi ya watoto wanaougua kisukari na badala yake kuwasaidia katika safari ya kudhibiti ugonjwa huo.

Kwa upande wake msimamizi wa idara ya magonjwa yasiyoambukiza katika Hospitali ya Rufaa ya Mafunzo ya Marsabit daktari Ann Sororo, amesema kuwa watoto 320 katika kaunti ya Marsabit wanaugua kusukari.

Amewataka wazazi kuhakikisha watoto wanaougua kisukari wanapata matibabu sahihi hospitalini ili kudhibiti hali yao.

Post Comment