Highlights

Wakazi wa wadi ya Loiyangalani wasusia ushirikishwaji wa bajeti ya ziada

NA Nyabande Orwa

Wakazi wa wadi ya Loiyangalani, kaunti ya Marsabit, wamesusia mkutano wa ushirikishwaji wa umma kuhusu bajeti ya ziada uliopangwa kufanyika leo Jumanne.

Baadhi ya wakazi waliozungumza na kituo hiki wameilaumu kamati ya bunge ya bajeti kwa kutofika katika eneo hilo wakati wa mchakato huo ili kujibu maswali yao kuhusu miradi ya maendeleo iliyotengewa fedha katika mwaka wa kifedha wa 2024/2025.

Kiongozi wa vijana wa Loiyangalani, Emanuel Emanman, amesema miradi kama ujenzi wa shule za chekechea na soko, ambayo ilipitishwa kupitia ushirikishwaji wa umma katika mwaka huo wa kifedha, bado haijaanza hadi sasa. Ameongeza kuwa hakuna kiongozi aliyejitokeza kutoa maelezo.

Akithibitisha tukio hilo, chifu wa eneo hilo John Orbora amesema kulikuwa na malalamiko kutoka kwa wakazi mapema leo wakati wa mkutano huo, lakini hawakusababisha vurugu. Kulingana na chifu huyo, wakazi wanalalamikia ukosefu wa uwazi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo baada ya mikutano ya ushirikishwaji wa umma na kamati za bunge.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment