Highlights

Gavana Mohamud Ali ahojiwa na seneti kuhusu ripoti ya ukaguzi wa fedha.

Na Samuel Kosgei

Gavana wa Kaunti ya Marsabit Mohamud Ali jana alifika mbele ya Kamati ya Seneti kuhusu Uwekezaji wa Umma wa Kaunti na Hazina Maalum (CPIC) kujibu maswali kuhusu ripoti ya ukaguzi wa hesabu ya mwaka wa fedha 2024/2025.

Wakati wa kikao hicho, maseneta walimuhoji kuhusu madai ya kasoro katika usimamizi wa fedha ndani ya Manispaa ya Marsabit, wakitaka ufafanuzi kuhusu matumizi ya fedha na hatua za uwajibikaji.

Gavana huyo alijibu maswali ya kamati hiyo, akitetea namna kaunti ilivyokuwa ikisimamia fedha zake huku akiahidi kushughulikia mapungufu yoyote yaliyoainishwa katika ripoti ya ukaguzi.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment