Highlights

Wavuvi Loiyangalani watakiwa kuwa makini dhidi ya mamba ziwani Turkana

NA JB Nateleng

Wito umetolewa kwa wavuvi wanaoendesha shughuli zao katika Ziwa Turkana, eneo la Loiyangalani kuwa waangalifu.

Haya yanakuja takriban wiki moja baada ya tukio ambapo mamba anasemakana kujaribu kuvamia wavuvi.

Wito huu umetolewa na mwenyekiti wa kitengo cha usimamizi wa ziwa hilo (BMU) Loiyangalani, Martin Losunyen ambaye amesema kwamba ni jukumu la kila Mvuvi kuhakikisha kwamba anajilinda na kuripoti tukio lolote la kuvamiwa na mamba katika shirika la kulinda wanyamapori (KWS) ili hatua stahiki ichukuliwa na mwathiriwa apate haki.

Pia Losunyen amewarai wavuvi kutumia zana bora za uvuvi ambazo haziwezi kuwaweka katika hatari ya kuvamiwa na mamba wanapoendesha shughuli yao ziwani.

Wakati uo huo mwenyekiti huyu ametoa onyo kali kwa wale wanaotumia watoto kuvua samaki, akisisitiza kwamba kitendo hicho ni kinyume cha sheria na yeyote atakayepatikana atawajibishwa kisheria.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment