Highlights

Asilimia 97 ya wanafunzi wamejiunga na gredi ya 10, Marsabit

NA Caroline Waforo

Asilimia 97 ya wanafunzi wa gredi ya 10 katika kaunti ya Marsabit wameripoti katika shule za sekondari ya juu, mwezi mmoja baada ya muhula wa kwanza wa mwaka 2026 kungoa nanga.

Kulingana na Mkrugenzi wa Elimu jimboni Marsabit Williams Kamugunah asilimia 72 ya wanafunzi hao wamejiunga na shule zilizoko kaunti ya Marsabit huku asilimia 25 ya wanafunzi hao wakijiunga na shule zilizoko nje ya kaunti hii.

Aidha Kamugunah amesema kuwa machifu na wasaidizi wao wanaendelea na msako ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wamejiunga na gredi ya 10 chini ya mtaala wa CBE

Vilevile ametoa wito kwa wazazi kuhakikisha wanao wanahudhuria masomo ili kufanikikisha asilimia 100 ya mpito wa gredi ya 10.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment