Highlights

wakristu watakiwa kuimarisha umoja na amani wiki hii kwa manufaa ya kujenga jamii imara.

Na JB Nateleng

Huku kanisa likianza wiki ya Umoja wa wakristu wiki hii, Wito wa ushirikiana na umoja umetolewa kwa wakristu pamoja na viongozi wa kanisa ili kujenga jamii imara na bora kwa vizazi vijavyo.

Mhashamu Baba Askofu wa Jimbo kuu katoliki la Nyeri Anthony Muheriaametoa wito kwamba ni jukumu la Wakristu kuweza kuliombea amani katika taifa la Kenya na ulimwenguni kote akiisifia umoja wa wakristu ambao unazidi kutia nguvu ushahidi wa kuwa wakristu wanaotetea haki na kusimama na ukweli.

Akizungumza na kituo hiki, Mkuu wa wito na kazi ya kitume katika Jimbo la Marsabit Padri Francis Mirgichan amesema kwamba ni wajibu wa kila Mkristu kuelewa mipango ya Mungu katika maisha yao, ili waweze kudumisha ushirikiana baina yao wenyewe.

Padri Mirgichan amewataka wakristu wote waliopokea Sakramenti ya Ubatizo kuweza kuwa katika mstari wa mbele wa kudumisha na kuendeleza mshikamano mwema  baina ya viongozi wa kidini, Viongozi wa kisiasa na wakristu wenzao.

Pia amewachangamoto wakristu kuweza kuungana na wakristu wengine kutoka madhehebu mbali ili kusaidia katika kuendeleza matendo mazuri ya utume.

Wiki ya kuombea umoja wa wakristo mwaka huu imebeba kauli mbiu kutoka katika kitabu cha Matendo ya Mitume  kifungu cha Biblia kinachowaingiza wakristu katika tafakari ya fadhila ya ukarimu.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment