Highlights

Gachagua Amshutumu Ruto kwa Kutotekeleza Ahadi Marsabit na ukanda wa kaskazini.

NA Samuel Kosgei

KIONGOZI wa chama cha DCP, Rigathi Gachagua, amezidisha mashambulizi dhidi ya Rais William Ruto akimtuhumu kwa kushindwa kutimiza baadhi ya ahadi alizotoa wakati wa ziara yake katika kaunti ya Marsabit mwaka wa 2023.

Akizungumza na wanahabari katika makao makuu ya chama hicho, Gachagua amesema rais aliahidi kushughulikia tatizo la umeme Marsabit, lakini hadi sasa kaunti hii bado haijaunganishwa na gridi ya umeme wa kitaifa.

Vilevile, amedai kuwa serikali imeshindwa kukomesha mila ya ukeketaji, akibainisha kuwa Marsabit bado ni miongoni mwa kaunti zinazoongoza kwa visa vya FGM licha ya ahadi ya kuumaliza kabisa.

Post Comment