Wachimba migodi waonywa dhidi ya uchimbaji haramu wa dhahabu katika machimbo ya Dabel
NA Caroline Waforo
Wachimba migodi wanaoendelea na shughuli za kusaka dhahabu kwa njia haramu katika migodi ya Hillo eneobunge la Moyale Kaunti ya Marsabit, wametakiwa kuondoka mara moja hadi wakati ambapo serikali itatoa mwongozo wa kufunguliwa kwa machimbo hayo.
Akizungumza na Shajara, Kamishna wa kaunti ya Marsabit James Kamau amesema kuwa oparesheni ya kuwaondoa wachimba migodi hao inaendelea akisema kuwa kwa sasa utulivu umerejea.
Hii ni kufuatia kisa ambapo mwanaume wa miaka 25 alifariki kutokana na majeraha ya kupigwa mawe baada ya mzozo kuibuka katika machimbo hayo siku ya Jumamosi iliyopita.
Wakati za ziara ya kiusalama katika kaunti ya Marsabit mwezi Mei mwaka 2025, waziri wa Usalama wa kitaifa Kipchumba Murkomen alisema kuwa migodi hiyo 13 itafunguliwa baada ya mikakati yote ya kiusalama kuwekwa ikiwemo ujenzi wa barabara.
Serikali kuu ilipiga marufuku shughuli katika migodi hiyo kufuatia utovu wa usalama japo shughuli katika machimbo hayo zimeripotiwa kuendelea.



Post Comment