Mwanaume mmoja afariki baada ya kufukiwa na mchanga katika machimbo ya Manyatta Daaba, Saku
NA Caroline Waforo.
Mwanaume mmoja amefariki dunia baada ya kufukiwa na mchanga katika machimbo ya Manyatta Daaba lokesheni ya Jirime eneo bunge la Saku.
Akithibitisha kisa hicho cha mapema leo Jumanne, OCPD wa Marsabit Central Beethoven Gachago amesema kuwa mwanaume huyo wa umri wa miaka 48 alifunikwa na mchanga huku juhudi za wenzake kujaribu kumnusuru zikiambulia patupu.
Gachago amewataka watu wanaoendesha shughuli hiyo kuchukua tahadhari.
Akizungumza mapema leo alipofika katika eneo la mkasa, chifu wa Lokesheni wa Jirime Enock Kallo amesema kuwa karibia watu 10 wamefariki katika machimbo hayo ya mchanga katika miaka ya hapo nyuma.
Wakati uo huo
Maafisa wa polisi wameanzisha uchunguzi kuhusiana na kisa ambapo nyumba yenye vyumba viwili imeteketea mapema leo katika kijiji cha Manyatta Konso lokesheni ya Dakabaricha.
OCPD Gachago amesema kuwa mmiliki wa nyumba hiyo ameeleza kukadiria hasara ya mali iliyokuwemo ndani ya nyumba hiyo pamoja na kiasi cha pesa ambacho hakijabainika hadi kufikia sasa.
Polisi wanafanya uchunguzi ili kubaini kiini cha moto huo.



Post Comment