Kituo cha kuwanusuru watoto chazinduliwa Loglogo
NA JB Nateleng
Kituo cha kwanza cha kuwanusuru watoto wanaokabiliana na dhulma za kijinsia, ikiwemo ukeketaji na ndoa za mapema kimezinduliwa leo Ijumaa katika eneo la Loglogo eneobunge la Laisamis kaunti ya Marsabit.
Kulingana na Alicia Leseper ambaye ni mmoja wa waanzilishi wa kituo hicho amesema kwamba ndoto ya kuanzisha kituo hicho kwa jina Loglogo Rescue Centre ilianza mwaka wa 2015 ambapo walitambua shida zinazowakumba watoto wa kike.
Alicia ameelezea kwamba kituo hicho kitasaidia katika kuwasaidia wasichana waathiriwa wa mila na tamaduni zilizopitwa na wakati.
Alicia amedai kwamba ukosefu wa makao salama kama haya unasababisha mwathiriwa kukosa haki.
Vilevile ameitaka jamii kutowatenga wasichana wanaopata mimba.



Post Comment