Highlights

Wavuvi na watumiaji wa ziwa turkana watakiwa kuwa waangalifu wakati wa upepo mkali ili kuepuka ajali.

NA Nyabande Orwa

Wavuvi na watu wanaotumia Ziwa Turkana wametakiwa kuwa waangalifu ili kuepuka ajali wakati wa upepo mkali. Akizungumza na kituo hiki, afisa wa uvuvi kutoka eneo la Loiyangalani, Abudo Huka, amesema matumizi ya rafta wakati wa upepo mkali huongeza hatari ya ajali kwa sababu ya muundo wake, hali inayoweza kusababisha wavuvi kuzama.

Huka ameongeza kuwa kutovaa jaketi za kuokoa maisha, matumizi ya dawa za kulevya wakiwa ziwani, pamoja na kubeba mizigo kupita kiasi, ni miongoni mwa sababu zinazosababisha vifo wakati ajali zinapotokea. Kauli yake imekuja saa chache baada ya Idara ya Hali ya Hewa kutoa tahadhari kwa wakazi wa Marsabit kwamba katika msimu huu wa kiangazi kasi ya upepo inaweza kuongezeka hadi noti 25, hali inayoweza kusababisha vumbi jingi, kupunguza uwezo wa kuona na kuathiri usafiri na shughuli za nje, hasa katika maeneo kame na nusu kame.

Post Comment