Watu zaidi ya elfu 128 marsabit wanahitaji msaada wa lishe na maji kutokana na kufeli kwa mvua za msimu uliopita.
NA Samuel Kosgei
Mamlaka ya kitaifa ya kukabili makali ya ukame NDMA tawi la Marsabit limesema kuwa zaidi ya watu elfu 128 wanahitaji msaada wa chakula na maji kutokana na uwepo wa ukame baada ya mvua za vuli kukosa kunyesha msimu jana katika mwezi wa October, November na December.
Akizungumza na idhaa hii ofisini mwake mkuu wa mawasiliano wa mamlaka hiyo John Ougo amesema kuwa Marsabit kwa sasa ipo katika hatua ya mwisho ili itagazwe kuwa katika hali ya hatari zaidi.
Anasema hali hii ya kuwa alert imechangiwa pakubwa na kufeli kwa mvua hizo ambazo zilikosa kunyesha.
Anasema kwa sasa wakaazi wengi katika jimbo hili wanahitaji msaada wa maji shughuli anayosema inaendelea kwa katika sehemu mbali mbali ikongozwa na serikali ya kaunti na washirika wake wa karibu kama vile Caritas na shirika la msalaba mwekundu – Redcross.
Kwenye suala la mifugo Ougo anasema mifugo wengi wameanza kuhamia sehemu za mbali ikiwemo nje ya jimbo ili kutafuta lishe na maji.
Aidha amewataka wakazi waanze kupuguza idadi ya mifugo ili kutosheleza mahitaji yake ambayo yanazidi kuongezeka ilhali maji na lishe yamepungua.



Post Comment