Highlights

Idara ya usajili wa watu Marsabit yalenga kusajili vitambulisho zaidi mwaka huu

Na Sabalua Moses

Idara ya usajili wa watu katika kaunti ya Marsabit imeimarisha mikakati ili kuhakikisha wakaazi zaidi wanapata vitambulisho vya kitaifa kabla ya uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2027.

Haya ni kulingana na mkuu wa usajili wa watu katika kaunti ya Marsabit Isaac Kibet ambaye amesema kuwa idara hiyo inalenga kusajili vitambulisho vingi mwaka huu wa 2026 ikilinganishwa na mwaka jana.

Aidha Kibet ameeleza kuwa kupitia ushirikiano na machifu idara hiyo imefanikiwa kuhakikisha kuwa vitambulisho vipya vinawafikia wananchi katika maeneo walioko.

Kulingana na Kibet Kaunti ya Marsabit ilirekodi ongezeko la usajili wa vitambulisho katika kipindi cha mwaka 2025 ambapo watu elfu 40,000 walituma maombi.

Post Comment