Afisa wa polisi ajitoa uhai Forolle
Na Nyabande Orwa
Afisa mmoja wa polisi amejiua kwa kujipiga risasi katika eneo la Forolle eneobunge la NorthHorr kaunti ya Marsabit.
Akithibitisha tukio hilo la mapema leo Jumanne, kamanda wa polisi kaunti ya Marsabit Leonard Kimaiyo, amesema kuwa afisa huyo alijipiga risasi kwenye kidevu kutumia bunduki aina ya AK-47 na kufariki papo hapo.
Kwa mujibu wa kamanda Kimaiyo, huenda afisa huyo aliyehudumu katika kituo cha polisi cha Forolle alijitoa uhai kutokana na msongo wa mawazo kufuatia mzozo wa kinyumbani.
Uchunguzi umeanzishwa mara moja kubaini chanzo kamili cha tukio hilo.



Post Comment