Sport Bulletins

Michuano Ya Kuwania Kombe La Ligi Kuu Nchini Uingereza Kuendelea Usiku Wa Leo

Picha;Hisani

By Waihenya Isaac,

Michuano Ya Kuwania Kombe La Ligi Kuu Nchini Uingereza Inatarajiwa Kuendelea Usiku Wa Leo Huku Mechi Mbili Zikiratibiwa Kugaragazwa.

WestHam United Ya Kocha David Moyes Itasaka Kuzidisha Shinikizo Katika Kumaliza Nne Bora Msimu Huu Baada Ya Kushinda Mechi Tatu Za Mwisho Walizocheza, Itakapomenyana Na WestBromich Albion Ugani Olympic Stadium Kuanzia Saa Tatu Usiku.

Itimiapo Saa Tano Na Robo Usiku Vijana Wa Kocha Brendan Rodgers Leicester City Watatafuta Nafasi Ya Kuchupa Hadi Katika Kileleni Mwa Jadwali La EPL Watakapovaana Na Chelsea Ugani King Power Stadium.

Leicester Wanashilikia Nafasi Ya Tatu Kwa Alama 35, Alama Mbili Nyuma Ya Viongozi Manchester United.

Aidha Chelsea Wamelala Katika Nafasi Ya 7 Wakiwa Na Alama 29 Baada Ya Kushiriki Mechi 18.

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter