Sport Bulletins

Jesse Lingard ataka Kusalia WestHam United.

By Waihenya Isaac,

Nyota wa klabu ya Westham United,Jesse Lingard amesema kuwa hana mpango wa kurejea kwenye klabu  yake ya Manchester United.

Lingard ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Westham kwa mkopo tangu mwezi Januari mwaka huu akitokea Klabu ya Manchester United yupo kwenye fomu nzuri kwa sasa, huku akitaja kufurahia kuichezea klabu ya hiyo.

Tangu kujiunga na Westham,Lingard amefanikiwa kufunga mabao tisa katika mechi 11.

Tayari klabu ya Westham United imetaja kuwa inapania kutoa kima cha pauni milioni 15 ili kumsajili kiungo huyo ambaye amesalia na mkataba wa mwaka mmoja ndani ya klabu  ya Manchester United.

Inaelezwa kuwa Lingard ameamua kuachana na klabu yake hiyo ya utotoni, kutokana na kocha wa sasa Ole Gunnar Solskjaer kutokuwa na imani naye.

Mbali na Westham, klabu za Arsenal, Inter Milan na Paris Saint Germain zimekuwa zikimtolea macho Lingard kuelekea msimu ujao.

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter