Sport Bulletins

Gor Mahia Yatemwa Nje Ya Kipute Cha Klabu Bingwa Barani Afrika CAF Champions League Na Klabu Ya CR Belouizdad Ya Algeria.

Picha;Hisani

By Waihenya Isaac.

Klabu Ya Gor Mahia Imebanduliwa Nje Ya Ya Michuano Ya Kuwania Kombe La Klabu Bingwa Barani Afrika CAF Champions League Na Klabu Ya CR Belouizdad Ya Algeria Kwa Jumla Ya Magoli Manane Kwa Moja.

Hii Ni Baada Ya Gor Mahia Kulazwa Jumla Ya Mogoli Mawili Kwa Nunge Katika Mechi Ya Finali Ya Kufuzu Katika Awamu Ya Makundi Ya Michuano Hiyo Hii Leo Katika Uga Wa Michezo Wa Nyayo Jijini Nairobi.

Gor Walikuwa Wa Kwanza Kucheka Na Wavu Kunako Dakika Ya 18 Kupitia Mshabualiaji Wa Burundi Jules Ulimwengu Kabla Ya CR Belouizdad Kutoka Nyuma Na Kushinda Mechi Hiyo.

Aidha CR Belouizdad Walisawazisha Kunako Dakika Ya 78 Kupitia Mchezaji Amir Sayoud Kabla Ya Hamza Bellahouel Kutia Kimiani Goli La Pili Na La Ushindi Kunako Dakika Ya 84.

Gor  Halmarufu Serekal Walikuwa Na Mlima Wa Kwenya Baada Yao Kupokezwa Kichapo Cha Magoli Sita Kwa Nunge Katika Mechi Ya Mkumbo Wa Kwanza Iliyochezwa  Disemba 26 Mwaka Jana  Katika Uwanja Wa August 20 1955 Stadium  Jijini Algiers.

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter