Sport Bulletins

Kocha Arsene Wenger Kurejea Uwanjani Emirates.

Kocha Arsene Wenger Akiwa Ugani Emirates.

Picha Hisani

By Waihenya Isaac.

Afisa Mkuu Mtendaji  Wa  Klabu Ya Arsenali Vinai Venkatesham Ameripotiwa Kuwasiliana Na Arsene Wenger Juu Ya Uwezekano Wa Kurudi Uwanjani Emirates.

Wenger Aliiongoza Arsenal Kutwaa Mataji Matatu Ya Ligi Kuu Na Vile Vile Kombe La FA Kabla Ya Kuondoka Baada Ya Miaka 22.

Meneja Huyo Mashuhuri Alijiuzulu Kutoka Wadhifa Wake  Mnamo Mwaka 2018 Baada Ya Miaka Yake Ya Mwisho Klabuni Kukumbwa Na Maandamano Na Hasira Kutoka Kwa Mashabiki Wa Klabu Hiyo.

Kocha Arsene Wenger Akiwa Ugani Emirates.Picha Hisani

Baada Ya Kuondoka Ugani Emirates,  Inasemekana  Kuwa   Kocha Arsene Wenger Aliapa Kutokanyaga Tena Uwanja Wa Emirates Ila Inaarifiwa Kuwa Afisa Mkuu Mtendaji Vinai Venkatesham Anafanya Njama Ya Kumrudisha.

Kwa Sasa Washika Bunduki Wamo  Katika Nafasi Ya 15 Kwenye Jedwali La Ligi Kuu  Nchini Uingereza Chini Ya Ukufunzi Wa Mikel Arteta Na Alama 13 Kutoka Kwa Mechi 11.

Arteta Anakabiliwa Na Shinikizo Baada Ya Kupoteza Mechi  4, Kushida  1 Na Kutoka Sare 1 Katika Mechi 6 Za Mwisho Za Arsenali Katika Ligi Ya Primia.

Comments are closed.

Subscribe to eNewsletter