Local Bulletins

Serikali Haitalegeza Kamba Kwenye Jitihada Zake Za Kumaliza Biashara Ya Dawa Za Kulevya Isiolo – Kamishna Herman Shambi

Kamishna Wa Kaunti Ya Isiolo Herman Shambi.
Picha;Hisani

By Samuel Kosgei,

Kamishna wa kaunti ya Isiolo Herman Shambi amesema kuwa serikali haitalegeza Kamba kwenye jitihada zake za kumaliza biashara na matumizi ya dawa za kulevya katika kaunti hiyo.

Akiongea Mjini Isiolo kamishna Shambi pia ameonekana kutamaushwa na idadi kubwa ya vijana ambao wamejitoza kwenye anasa na starehe za dunia

Hata hivyo Shambi amesema kwamba vita dhidi ya mihadarati si jukumu la serikali pekee bali inahitaji ushirikiano kati ya serikali na wananchi

Kando na hayo kamishina Shambi ametoa wito kwa viongozi walio mamlakani kuwasaidia vijana kupata liseni za boda au uendeshaji wa mashine za ujenzi ili kusaidika na nafasi za kazi kutoka kwa serikali kama vile barabara ya Isiolo kwelekea Mandera

One Comment

  1. Hey very nice web site!! Man .. Excellent .. Amazing .. I will bookmark your web site and take the feeds also…I’m happy to find numerous useful info here in the post, we need develop more strategies in this regard, thanks for sharing. . . . . .

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter