Waziri wa ulinzi Soipan Tuya ataka jamii kusuluhisha mzozo wa ardhi za jamii na KDF kwa njia ya mazungumzo.
SERIKALI imeitaka jamii zinazoishi karibu na kambi ya jeshi nchini kutokuwa na migogoro ya mahusiano na wanajeshi kwani mara nyingi jeshi inalenga kuimarisha usalama wa mpaka wa Kenya na hata jamii za eneo husika.
Waziri wa ulinzi nchini Soipan Tuya akizungumza kwenye kongamano la kujadili haki na usajili wa ardhi ya jamii iliyoandaliwa jijini Nairobi na shirika la IMPACT, amesema jeshi mara nyingi haina ubaya wowote na ardhi ya jamii bali lengo kuu ni kukuwa tayari katika ulinzi wa mipaka. Anasema pia mara kwa mara hatua za kutwaa ardhi za jamii hazipitii kwenye wizara ya ardhi kutokana na hali ya uzito wa sera za ulinzi.
Hata hivyo Waziri Soipan amesema kuwa ardhi hizo za kijamii kama vile katika eneo la Karare kaunti ya Marsabit na maeneo mengine wakaazi wanahusishwa ili waruhusu jeshi wa kujenga kambi yao.
Anasema kamati maalumu iliundwa katika idara ya jeshi ili kutatua mizozo ya kijamii inayoibuka kutokana uwepo wa jeshi.
Ameongeza pia kuwa ni jukumu la KDF kusaidia jamii za karibu katika kuanzisha maendeleo na msaada mwingine wowote unaowezekana.
Kwa muda wakaazi wa Karare kaunti ndogo ya Saku wamekuwa wakalalamika kunyakuliwa kwa ardhi ya kijamii ekari 2500 na idara ya jeshi nchini KDF hatua iliyowahi kusababisha wao kupeleka maombi bungeni ila suala hilo kutatuliwa.
Jamii inadai kuwa eneo hilo ni lao la malisho, eneo la kitamaduni na vyanzo vya maji, na kwamba KDF ilipuuza eneo mbadala walilopendekeza la Kubi Kalo. Mgogoro huu umeendelea tangu mwaka 2019.



Post Comment