Washukiwa wawili wa ukeketaji kule Moyale wanasubiri uamuzi wa dhamana.
Washukiwa wawili wanaotuhumiwa kuhusika katika ukeketaji wa wasichana watatu wenye umri wa miaka 13, 10 na 9 kule Moyale, wanatarajiwa kujua iwapo wataachiliwa kwa dhamana siku ya Ijumaa tarehe 28 mwezi huu.
Washukiwa hao Sire Bante, 68, na baba wa watoto hao, ShariffBonaya, waliokamatwa na kufikishwa mahakamani tarehe 11 Novemba, ambapo walikana mashtaka.
Wawili hao wanakabiliwa na mashtaka ya kufanya ukeketaji, kushindwa kuripoti kisa hicho, na kuandaa kutekeleza kitendo hicho. Upande wa mashtaka umepinga dhamana, ukisema huenda washukiwa waka wakawashawishi mashahidi, jambo ambalo linaweza kuathiri mchakato wa kesi.



Post Comment