Highlights

Wakazi wa Marsabit wamehimizwa kuangalia kwa makini aina ya chakula wanachokula ili kuepuka kupata vidonda vya tumbo (ulcers).

Wakazi wa Marsabit wamehimizwa kuangalia kwa makini aina ya chakula wanachokula ili kuepuka kupata vidonda vya tumbo (ulcers).

Wito huu umetolewa na afisa wa afya kutoka hospitali ya rufaa na mafunzo ya Marsabit, Steve Sereti, ambaye anasema kuwa mara nyingi vyakula tunavyokula husababisha vidonda tumboni, na vidonda hivyo vikikosa kutibiwa mapema vinaweza kuleta matatizo makubwa kama saratani ya utumbo.

Akizungumza na idhaa hii, Sereti amesema kuwa ingawa bado haijathibitishwa moja kwa moja kuwa vidonda vya tumbo husababisha saratani ya tumbo, ni muhimu watu wawe waangalifu na chakula wanachokula. Amewataka wakazi wajiepushe na vyakula vyenye asidi nyingi.

Sereti ametaja dalili kama kuumwa na tumbo ukiwa hujala kwa muda mrefu, pamoja na kutapika chembe za chakula, kuwa ishara za uwezekano wa kidonda cha tumbo.

Ameongeza kuwa vidonda vya tumbo vinaweza kutibiwa ikiwa mgonjwa atafuata ushauri wa daktari. Pia amewahimiza wakazi kutembelea vituo vya afya mapema wanapohisi hali zao hazibadiliki ili kupimwa zaidi.

Post Comment