Kamanda wa polisi Marsabit awahakikisha wakazi usalama msimu wa sherehe za disemba ukikaribia.
NA NYABANDE ORWA
Kamanda wa polisi wa kaunti ya Marsabit, Leonard Kimaiyo, amesema kuwa usalama umeimarishwa kikamilifu katika kaunti hii huku msimu wa sherehe za Krismasi ukikaribia.
Akizungumza na kituo hiki afisini mwake, Kimaiyo amesema maafisa wa usalama wataongeza doria ili kukabiliana na wahalifu wanaolenga kuvuruga amani ya kaunti.
Wakati huohuo, Kimaiyo amewataka madereva kuwa waangalifu barabarani na kuepuka matumizi ya pombe na dawa za kulevya wakati wa kuendesha magari, ili kupunguza visa vya ajali.
Kuhusu usalama wa jamii, Kamanda Kimaiyo amewahimiza wakazi kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama pindi wanapoona tukio lolote la kuvunja sheria.
Aidha, amewashauri raia kuwajulisha majirani zao wanapoondoka kusafiri, ili kusaidia kuzuia wizi wa mali kwenye biashara na nyumba za watu.



Post Comment