Diocese of Marsabit, Local Bulletins

Warsha ya siku tatu ya kutoa mafunzo ya kidini kwa walimu wa watoto wa kanisa katoliki PMC yangoa Nanga.

Watawa wa kike pamoja na walimu wa watoto wa kanisa katoliki PMC katika jimbo la Marsabit wakipokea mafunzo.
Picha:Isaac Waihenya

By Waihenya  & Qabale,

Warsha ya siku tatu ya kutoa mafunzo ya kidini kwa walimu wa watoto wa kanisa katoliki PMC katika jimbo la Marsabit imengoa nanga rasmi hii leo.

Warsha hiyo ambayo inaongozwa na mratibu wa maswala ya vijana katika kanisa katolika jimboni Marsabit Sister Agatha Katuma Mativo inapania kuwapa elimu walimu hao kuhusiana na jinsi ya kuwaongoza watoto ambao ndio viongozi wa kesho.

Akizungumza na Radio Jangwani Sister Agatha ameitaja hafla hiyo ambayo imewaleta pamoja walimu 62 kutoka parokia zote hapa jimboni kuwa ya manufaa kwa walimu pamoja na wananafuzi wao.

Watawa wa kike pamoja na walimu wa watoto wa kanisa katoliki PMC katika jimbo la Marsabit wakipokea mafunzo.
Picha:Isaac Waihenya

Kwa upande wake msimamizi wa maswala ya kitume katika kanisa katoliki jimbo la Marsabit Padre Tito Makhoha ni kuwa ni jukumu la kila mmoja kumtumikia Mungu katika njia zote.

Padre Tito amewataka walei hao kuwa katika mstari wa mbele kwenye kuhakikisha kuwa injili inasonga mbele huku wakiwafunza watoto njia ya imani.

Warsha hiyo pia inahudhuriwana baadhi ya watawa wa Kike kutoka hapa jimboni Marsabit.

Subscribe to eNewsletter