County Updates, Diocese of Marsabit, Local Bulletins

KCPE 2020 – Wazazi Watakiwa Kujukumikia Elimu Ya Watoto Wao.

By Adano Sharawe,

Wazazi na wanafunzi kutoka kaunti ndogo ya Laisamis wanasherehekea matokeo bora ya mtihani wa KCPE mwaka huu, wengi wao wakiwa wamepata alama 300 na zaidi.

Hata hivyo, walielezea masikitiko yao ya kushuka kwa matokeo hayo kulinganisha na mwaka 2019.

Kulingana na mzazi Edward Delea, janga la corona liliwakoroga wanafunzi wao ila walijikaza kufa kupona.

Edward ambaye ni daktari ni babake mwanafunzi bora katika shule ya msingi ya Laisamis Valgelista Kulmise Delea ambaye alipata alama 365.

Mwanafunzi bora katika shule ya msingi ya Laisamis Valgelista Kulmise Delea (katika) akiwa pamoja na wazazi wake.
Picha:Radio Jangwani

Kulingana na mzazi huyo ni kuwa changamoto za kuhamahama kwa wafugaji pia zimechangia watoto wengi kupata matokeo ambayo hawakutarajia.

Amesema wakati huu ambapo shule zimefungwa wazazi wanapaswa kujukumika kama inavyopaswa kwa kufuatilia maendeleo ya elimu ya wanao.

Kwa upande wake Delea amesema kwamba kupitia ushirikiano mwema wa walimu pamoja na wazazi na kuzidi kuwa na nidhamu kumemsaidia kufanya vyema katika mitihani hiyo.

Delea amesema ana ndoto ya kuwa wakili.

Mwanafunzi Bora Katika Shule Ya Msingi Ya Laisamis Valgelista Kulmise Delea Ambaye Alipata Alama 365.
Picha:Radio Jangwani

Naye mamake Delea, Francisca Delea ambaye ni mwalimu wa shule ya upili amewataka wazazi kulea vyema watoto wa kike ili kuwasaidia kumaliza masomo yao na kuwa watu wa manufaa katika jamii.

Waziri wa elimu Profesa George Magoha akitangaza matokeo hayo alisema wanafunzi wote waliofanya mtihani huo watajiunga na shule za upili.

Shilingi bilioni nane kulingana na waziri Magoha, zimetengwa ili kuboresha miundo mbinu katika shule za upili kwenye kaunti ndogo 110 kote nchini ili kuwezesha wanafunzi wote waliofanya mtihani wa KCPE kujiunga na shule za upili.

Aidha Mwafunzi katika kaunti ndogo ya Laisamis ni  Nashipai Baru Chana kutoka shule ya msingi ya Tereem katika eneo la Korr aliyejizolea alama 382.

Subscribe to eNewsletter