Local Bulletins

Askofu Michael Otieno Odiwa Asimikwa Rasmi Na Kama Askofu Wa Kanisa Katoliki Jimbo La Homabay

Picha;Hisani

By Samuel Kosgei,

Askofu Michael Otieno Odiwa alisimikwa rasmi na kama Askofu wa kanisa Katoliki jimbo la Homabay Jumanne, baada ya uteuzi wake mwaka jana. Sherehe ya kusimikwa kwake ilifanyikia katika shule ya upili ya Homabay Boys.

Hafla hiyo ya kumtawaza Askofu Odiwa iliongozwa na mwakilishi wa Papa humu nchi Kenya Askofu Mkuu Nuncio Bert Van Megen ambaye alimtaja askofu Odiwa kama mhubiri aliyefanya kazi yake bila kutetereka na kumtumikia Mungu kwa roho moja kulingana na mafunzo ya kanisa Katoliki.

Amesema kuwa alipompigia simu Askofu Odiwa kumpa habari hiyo nzuri mwaka jana, Odiwa alishangazwa na kutoamini mara moja habari hiyo ya kuteuliwa kuwa askofu wa homabay na Papa Francis.

“Mbona mimi? Aliuliza Odiwa kwenye simu nikimpa taarifa za kuteuliwa kwake. Nilimsisitizia kuwa wengi wameona Imani na vigezo vyako vya kuweza kuwa Askofu wa jimbo la Homabay, na Papa mwenyewe amekubali kukuteua, kimya kirefu kilitawala kwa muda asijue anijibu nini” alisema mwakilishi wa Papa Askofu Mkuu Bert Van Megen

Aidha, Nuncio Van Megen alisema, kama tu Jeremiah alivyoandaliwa na Mungu akiwa tumboni mwa mamake ili amhudumie ndivyo anavyosema kuwa alimrai Askofu Odiwa akubali wito wa kutakiwa awe askofu wa Homabay akisema ni mapenzi ya Mungu yeye kuchaguliwa.

Mtakatifu Papa Francis  kwenye ujumbe kwa Askofu Odiwa amesema, “Wewe mwanangu mpendwa umeonekana kuwa unaweza kutumiza kazi hiyo kulingana na uangalifu na bidii yako ya kichungaji na tabia zako ya kipekee za kiutu na za upadre”.

Ameendelea kusema “baada ya kuzingatia ushauri wa kutoka kwa ‘congregasio’ ya uenezaji wa Imani kwa taifa tunakusimika kuwa Askofu wa kanisa kuu la Homabay” Taarifa ya Papa imesema kupitia ujumbe uliosomwa na mmoja wa maaskofu waliokuwa kwenye hafla hiyo.

Wakti uo huo kwenye mahubiri yake ametoa tahadhari kwa baadhi ya wahubiri wanaotumia makanisa kama ngazi ya kujinufaisha pekee yao akisema hawatafaulu katika mienendo yao kwani wanapotosha kondoo wa Mungu badala ya kuwaongoza.

Picha;Hisani

Uteuzi wake Askofu Michael Odiwa ulifanywa na Mtakatifu Papa Francis Mjini Rome Jumapili ya tarehe 29th, November 2020.

Odiwa alizaliwa mnamo mwaka wa 1962, katika kijiji cha Sori kaunti ya Homabay. Alibatizwa mwaka 1963 katika Parokia ya Migori na kutawazwa kuwa shemasi mwaka wa 1992 huku akifanywa kuwa padre wa kanisa katoliki jimbo la Homa Bay mwaka wa 1993.

Amekuwa akihudumu kama Padre katika jimbo kuu la Adelaide nchini Australia.

Subscribe to eNewsletter