Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na Joseph Muchai,
Zoezi la kutoa chanjo ya polio kwa watoto katika kaunti ya Marabit imeng’oa nanga hii leo.
Chanjo hiyo inalenga watoto wa umri wa chini ya miaka 11 katika maeneo bunge yote manne ya kaunti ya Marsabit.
Akizungumza na Radio Jangwani kwa njia ya simu mratibu wa huduma za utaoaji chanjo katika kaunti ya Marsabit Abdi Boru amesema kuwa wanalenga kuwachanja watoto wote walio chini ya umri wa miaka 11 ili kuwalinda dhidi ya ugonjwa wa Polio.
Aidha Boru amesema kuwa zoezi hilo limechochewa mlipuko wa wa ugonjwa wa polio nchini Ethiopia ambao umelazimu serekali kuchukuwa hatua za dharura ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo hapa nchini.
Kadhalia afisa huyu wa afya amewarai wazazi kuhakikisha kuwa wanao wamepata chanjo hiyo kwani inawaondolea hatari ya kupatwa na ugonjwa wa Polio.